• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yaisifu China kwa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na kesi ya chanjo

    (GMT+08:00) 2018-07-25 21:06:39

    Shirika la Afya Duniani WHO leo limesema, linaunga mkono hatua zilizochukuliwa na serikali ya China katika kukabiliana na kesi ya chanjo.

    Taarifa iliyotolewa leo na Shirika hilo imesema, WHO inasubiri matokeo ya uchunguzi zaidi, na kuwa iko tayari kutoa msaada kwa idara ya afya ya China.

    Baraza la serikali ya China limeunda kikundi maalumu cha uchunguzi wa kesi ya Shirika la changjo la Changsheng la mjini Changchun kutengeneza chanjo bandia ya Rabies. Awali, rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu Bw. Li Keqiang waliagiza uchunguzi wa kina juu ya kesi hiyo ufanyike ili kuhakikisha afya ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako