• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China achangia mawazo kuhusu mwongo ujao katika kongamano la biashara la BRICS

    (GMT+08:00) 2018-07-26 00:40:36

    Rais Xi Jinping wa China amechangia mawazo yake kuhusu mabadiliko ambayo dunia inakwenda kushuhudia katika mwongo ujao.

    Akizungumza kwenye kongamano la biashara la kundi la BRICS linalojumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini lililofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi amesema mwongo ujao utakuwa muhimu sana ambapo waendeshaji wapya wa uchumi wa dunia watachukua nafasi ya wale wa zamani, mabadiliko ya kasi yatatokea kwenye mandhari ya kimataifa na muungano wa nguvu za kimataifa. Pia amesema dunia itashuhudia kujipanga upya kwa mfumo wa utawala wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako