• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waafrika Kusini waichukulia ziara ya rais wa China kama alama ya uhusiano imara wa nchi mbili

    (GMT+08:00) 2018-07-26 07:50:26

    Watu wa Afrika Kusini wameichukulia ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Afrika Kusini kuwa alama ya uhusiano imara wa kidiplomasia kati ya nchi mbili.

    Ikulu ya Afrika Kusini imesema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ziara hiyo imefanyika kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimataifa kati ya Afrika Kusini na China.

    Mchambuzi wa siasa Somadoda Fikeni anaona ziara hiyo itazidisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa kundi la BRICS na zina uhusiano mzuri wa kisiasa, ambao umeshuhudiwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na shughuli nyingine za kiuchumi.

    Msemaji wa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini Bw. Khusela Diko amesema nchi hizo mbili zina uhusiano mzuri wa kihistoria na kimkakati, ambao umeinuka na kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.

    Na mtafiti mwandamizi wa sera za kigeni Bw Jacobus van Staden amesema nchi hizo mbili zinatumia ziara hiyo kuandaa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika baadaye hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako