• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujiuzulu Oezil timu ya taifa kwazua zogo Ujerumani

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:04:02
    Hatimaye zogo, lawama na mijadala mikali imezuka nchini Ujerumani, baada ya mchezaji wa timu ya taifa hilo Mesut Oezil kuamua kujizulu kutoka timu ya taifa ya Ujerumani.

    Gazeti la Sueddeutsche Zeitung la Ujerumani limeeleza uamuzi wa mchezaji huyo kuwa ni kipigo kamili cha majira ya joto, wakati mtaalamu maarufu wa soka la Ujerumani Raphael Honingstein ameandika kuhusiana na kujiuzulu Oezil kutoka katika timu ya taifa kuwa ni hali mbaya kuliko kushindwa kokote katika kombe la dunia.

    Naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel amemshukuru Mesut Oezil kwa mchango wake katika timu ya hiyo ya taifa ya Ujerumani.

    Kiungo huyo amestaafu soka ya kimataifa akilalamikia kufanyiwa ubaguzi na chama cha soka Ujerumani baada ya kutolewa mbuzi wa kafara baada ya timu hiyo kutolewa mapema kwenye fainali za michuano ya kombe la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako