• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Angola yaendelea kuwa njia ya usafirishaji wa pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:15:23

    Waziri wa raslimali za misitu wa Angola Bw. Andre Moda amesema Angola inaendelea kukabiliwa na changamoto ya kuwa njia ya mpito ya usafirishaji wa pembe za ndovu, faru, magamba ya kakakuona, Sokwe na ndege pori.

    Akiongea mjini Luanda kwenye mkutano wa pili wa wataalam kuhusu utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika kupambana na biashara haramu ya wanyamapori, Bw. Moda amesema mwaka jana peke yake Angola ilikamata tani 1.2 za pembe za ndovu na sehemu ya wanyama wengine kutoka kwa majangili.

    Amesema mpaka mrefu wa nchi hiyo, unafanya kuwe na mahitaji ya pesa na kuimarisha ukaguzi na udhibiti.

    Angola inaandaa mkutano huo kwa mara ya pili, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mkakati wa ulinzi wa wanyama pori na ushiriki wa Afrika kwenye mkutano ujao kuhusu biashara ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka, utakaofanyika mwezi Mei mwakani mjini Colombo, Sri Lanka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako