• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wazindua mpango wa kuhimiza ufufuaji wa miji ya Kenya

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:15:42

    Umoja wa mataifa umezindua mpango wa kuhimiza ukuaji endelevu wa miji huku miji hiyo ikikabiliwa na changamoto za uchafuzi wa hewa, uhalifu na kupanuka kwa makazi haramu.

    Mkurugenzi wa shirika la makazi la Umoja wa mataifa Bibi Maimunah Sharif, amesema mkakati huo utakaotekelezwa kati ya mwaka huu na mwaka 2021 utakuwa muhimu katika kufanikisha ufufuaji wa miji ya Kenya.

    Bibi Sharif amesema mpango huo utatoa mwongozo kwenye kuboresha usimamizi wa ardhi na makazi endelevu yaliyopangwa, na kuwepo kwa huduma bora za mjini na miundombinu.

    Waziri wa usafirishaji na miundo mbinu wa Kenya Bw. James Macharia amesema mpango huo wa Umoja wa mataifa una lengo la kuhimiza wadau wa serikali na wasio wa serikali, kuhimiza uwepo wa makazi endelevu kuwa na mpango wa taifa wa maendeleo na mipango miji, ulio na ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako