• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kutoa vibali vya kazi kwa wawekezaji wageni ndani ya siku 14

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:16:02

    Mamlaka nchini Tanzania zimesema vibali vya kufanya kazi kwa wawekezaji wa kigeni wanaotaka kuanzisha biashara sasa vitatolewa ndani ya wiki mbili.

    Naibu waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, ajira, vijana na walemavu Bw. Anthony Mavunde, amesema kama mwombaji ana nyaraka zote zinazotakiwa, kibali chake kitakuwa tayari ndani ya siku 14. Amesema huko nyuma hakukuwa na muda maalum wa serikali kutoa vibali vya kazi. Amesema kwa sasa serikali inatekeleza mpango uliopitishwa hivi karibuni wa kuboresha mazingira ya biashara.

    Mwenyekiti wa chama cha wahudumu wa utalii cha Tanzania TATO Bw. Willy Chambulo, amesema ilikuwa vigumu kwao kurefusha vibali vya wafanyakazi wao, na kuathiri utoaji wao wa huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako