• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya IS mkoani Sweida kusini mwa Syria yafikia 215

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:19:04

    Watu 215 wameuawa na wengine 180 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mfululizo yaliyofanywa na kundi la Islamic State mkoani Sweida, kusini mwa Syria. Shirika la haki za binadamu la Syria limesema wapiganaji 30 wa IS, wakiwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga, wameuawa kwenye mashambulizi hayo. Jeshi la Syria, likisaidiwa na wakazi wa mji huo, limefanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa IS kutoka kwenye baadhi ya maeneo waliyoingia.

    Mashambulizi hayo ya IS yamekuja wakati jeshi la Syria linashambulia vikali vituo vya IS magharibi mwa mkoa wa Daraa, karibu na Milima ya Golan inayokaliwa na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako