• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM asikitishwa na vifo vya watu 80 kwenye moto wa msituni Ugiriki

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:19:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa wa wahanga na serikali ya Ugiriki, baada ya moto wa msituni kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80 nchini humo. Bw. Guterres amesema Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA inafuatilia maendeleo ya maafa hayo, na kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya Ugiriki na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na maafa hayo.

    Jumatatu asubuhi, moto ulianza kwenye mlima Penteli kwenye peninsula ya Attica nchini Ugiriki, na ukaenea haraka hadi pwani na kuwafanya maelfu ya watu kukimbia makazi yao. Mameya wa eneo hilo wanahofia kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka wakati kazi ya uokoaji inaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako