• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaru vya Israel vyavamia Gaza mashariki na kuwaua wapiganaji watatu wa Hamas

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:19:48

    Vifaru vya Israel vimeshambulia kwa mizinga vituo vya chama cha Hamas karibu na mpaka kati ya Gaza mashariki na Israel, na kuwaua wapiganaji watatu wa kundi hilo. Maofisa wa usalama huko Gaza wamesema vifaru vya Israel vilishambulia kwa mizinga vituo vinne vya Brigedi ya al-Qassam, tawi la jeshi la Hamas.

    Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hatua hiyo inalenga kujibu shambulizi lililotokea mapema dhidi ya kikosi cha jeshi la Israel kilichokuwa mpakani, ambalo limejeruhi askari mmoja wa Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako