• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aahirisha mkutano ujao kati yake na Putin hadi mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2018-07-26 09:20:32

    Ikulu ya Marekani imesema mkutano ujao kati ya rais Donald Trump na mwenzake wa Russia Vladimir Putin utaahirishwa mpaka mwaka kesho, baada ya uchunguzi kuhusu Russia kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 kumalizika.

    Wiki iliyopita Ikulu ya Marekani imesema Rais Trump alimtaka mshauri wake Bolton kumwalika rais Putin mjini Washington mwishoni mwa mwaka huu, na kwamba maandalizi ya mkutano huo yameshaanza. Lakini Ikulu ya Russia imekanusha habari hiyo na kusema Trump na Putin wanaweza kukutana kando ya mikutano ya kimataifa, na hakuna maandalizi ya mkutano mwingine kati yao mjini Washington.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako