• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia kurekebisha mfumo wa elimu na kuufanya uendane na sifa ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2018-07-26 10:02:03

    Somalia inapanga kuufanyia mageuzi mfumo wake wa elimu kuanzia mwezi ujao, ikiwa ni ni pamoja na uzinduzi wa mfumo mpya, na kuiweka lugha ya kisomalia kuwa lugha ya kufundishia kwenye shule za msingi.

    Mshauri wa wizara ya elimu ya nchi hiyo anayesimamia utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu Bw. Mohamed Abdulkadir, amesema chini ya mfumo mpya unaoitwa mfumo wa 4-4-4, wanafunzi watatumia miaka minne kwenye elimu ya msingi, miaka minne kwenye elimu ya msingi ya juu na miaka minne mingine kwenye shule ya sekondari kabla ya kuweza kuandikishwa kwenye shule za elimu ya juu.

    Bw. Abdulkadir pia amesema, katika miaka 30 iliyopita, Somalia imekuwa na hamu ya kuwa na mfumo wa elimu wa kienyeji unaolingana na hali ya nchi, na hatimaye wamepata mfumo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako