• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo vinavyotokana na mapigano katikati ya Ethiopia yafikia 11

    (GMT+08:00) 2018-07-26 10:02:22

    Mkuu wa ofisi ya mawasiliano ya serikali ya jimbo la Oromia ya Ethiopia Bw. Negeri Lencho ametoa taarifa ikisema, idadi ya vifo vinavyotokana na mapigano yaliyotokea wikiendi iliyopita katika jimbo la Oromia, katikati ya Ethiopia imeongezeka hadi 11.

    Bw. Lencho amesema, mapigano hayo yaliyotokea katika mji wa Goba ulioko umbali wa kilomita 416 kutoka Addis Ababa, yamesababisha vifo vya watu 11 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa. Pia amesema, vikosi vya usalama vya jimbo na taifa vimetumwa kwenye mji huo kuzuia mapigano yasitokee tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako