• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuboresha zaidi sera ya kufungua mlango na kuongeza ajira

    (GMT+08:00) 2018-07-26 18:34:15

    Ofisa mwandamizi wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China jana amesema, China itaboresha zaidi sera ya kufungua mlango, ili kurahisisha utaratibu wa uwekezaji wa nchi za nje, na kuongeza ajira.

    Kutokana na waraka uliotolewa na idara kadhaa husika, China itafungua mlango zaidi katika sekta ya huduma, na kuhamasisha mauzo ya huduma za utamaduni, utalii, elimu, ujenzi, tiba ya jadi ya kichina na ubunifu katika nchi za nje. Wakati huo huo, China pia itahimiza kampuni za nchi za nje kuwekeza katika sehemu za magharibi na kati, na kaskazini na mashariki nchini China, ili kuongeza ajira katika maeneo hayo.

    Aidha, China itarahisisha utaratibu wa uwekezaji wa nchi za nje, na kulinda maslahi halali ya wawekezaji kutoka nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako