• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikwazo vya biashara vyaongeza athari mbaya kwa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-26 19:14:24

    Mkurugenzi mkuu wa shirika la Biashara Duniani WTO Bw. Roberto Azevedo amesema, kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara hakutasaidia ongezeko la uchumi la dunia wala kutoa fursa za ajira, hivyo pande zote zinapaswa kuliunga mkono shirika la WTO kwa kuweka kipaumbele msimamo wa kufungua mlango.

    Akiongea na wanahabari huko Geneva Bw. Azevedo amesema ripoti mpya iliyotolewa na shirika hilo kuhusu biashara ya dunia imeonesha, hatua za vikwazo vya kibiashara zikiwemo kuongeza ushuru, kuweka vizuizi na usimamizi mkali wa forodha zimeongezeka hivi karibuni.

    Bw. Azevedo amezitaka pande zote husika zibadilishe msimamo wao na kutafuta mpango wa utatuzi. Shirika la WTO litaendelea kufanya majadiliano na pande zote, kueleza matokeo ya hatua zote za biashara, na kutoa misaada katika sekta za mipango na kanuni kwenye msingi wa kufikia makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako