• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani na Umoja wa Ulaya zakubali kufanya mazungumzo kutuliza mkwaruzano wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-07-26 19:18:52

    Marekani na Umoja wa Ulaya zimekubali kufanya mazungumzo ili kutatua vikwazo na mkwaruzano wa kibiashara kati yao. Pia pande hizo mbili zimeamua kuacha kuongeza ushuru mpya kwa muda. Lakini malengo hayo bado yanakabiliwa na changamoto nyingi.

    Baada ya kuzungumza na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Jean-Claud Juncker katika ikulu ya Marekani, rais Donald Trump wa Marekani amesema, pande hizo mbili pia zimekubali kuongeza ushirikiano katika sekta ya nishati, ambapo Umoja wa Ulaya unatarajia kuingiza gesi asilia zaidi.

    Bw. Juncker amesema, mazungumzo yajayo yatasaidia kusimamisha kwa muda ushuru mpya kwa bidhaa za pande mbili na kutathmini tena ushuru wa chuma na alumini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako