Kwa mujibu wa afisa mkuu wa kampuni hiyo, Paul McDade amesema maandamano ya wakaazi wakitaka manufaa ya moja kwa moja ya asilimia 5 ya mradi huo katika eneo hilo yametia hofu kazi zao .
Hata hivyo, ameahidi kwamba wataendelea na oparesheni zao pindi tu tatizo hilo litakaposuluhishwa.
Tullow inalenga kufikisha mapipa laki moja ya mafuta kwa siku kufikia mwaka 2021 -22.
Kwa sasa inasafirisha mapipa 600 kila siku hadi katika bandari ya Mombasa swala ambalo wanakijiji wameanza kulipinga kwa kudai fedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |