Maamuzi haya yanajiri baada ya kushuhudiwa kwa kasoro ya sukari nchini Kenya iliyochangia wafanyibiashara kukimbilia soko hilo.
Hatua hiyo sasa imechangia kuongezeka kwa bei ya sukari nchini Uganda kwani sukari nyingi imeishilia Kenya.
David Kiiza afisa katika wizara ya biashara Uganda amesema watahakikisha marufuku hayo yanatekelezwa kwani zaidi ya tani elfu 25 za sukari zimeuzwa nje ya nchi .
Amesisitiza kwamba wataruhusu tani elfu 10 pekee za sukari kuuzwa nje .
Upande mwengine wafanyibiashara wa sukari wamejitetea wakisema Uganda ina sukari ya kutosha na uuzaji wa sukari nchini Kenya hautaathiri bidhaa hiyo sokoni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |