Abiy atakwenda Washington DC na Los Angeles katika ziara ya siku 6 itakayolenga kuimarisha uhusiano baina nchi hizo 2 .
Kiongozi huyu aliyeingia mamlakani mwaka huu Aprili aidha ameahidi kuendelea kujenga uhusiano bora na nchi za Afrika ili kuimarisha uchumi na maendeleo ya jamii ya Ethiopia.
Hivi majuzi Abiy Ahmed amekutana na viongozi wa Eritrea ili kuregesha uhusiano wa kidiplomasia .
Wiki jana rais a Eritrea Isaias Afwerki alifanya ziara ya kihistoria nchini Ethiopia na mataifa hayo mawili yaliandika historia kwa kuanzisha uhusiano mpya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |