• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:shughuli za uchimbaji madini kusitishwa

    (GMT+08:00) 2018-07-26 19:42:24

    Naibu waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameiagiza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya RAK inayochimba madini ya kaolin yanayotumika kutengeneza marumaru kusimamisha shughuli zake kwa siku mbili ili kujiridhisha thamani halisi ya madini hayo.

    Nyongo ametoa agioz hilo alipofanya ziara katika Kijiji cha Kimani wilayani Kisarawe mkoani Pwani, ambalo ni eneo linalochimbwa madini hayo.

    Amesema haitwazekana serikali ipate mrabaha wa asilimia tatu ya shilingi 3,000 kwa tani wakati wao katika tani wanazalisha 'tiles' nyingi na wanauza kwa bei ya juu kwa wananchi..

    Huenda mkataba wa kampuni hiyo kwa kuwa yenyewe ilishindwa kuchimba kutokana na kutokuwa na uwezo na hivyo kuingia mkataba na kampuni nyingine ambayo ndiyo huwalipa Sh 3,000 kwa tani kiasi ambacho ni kidogo ikilinganishwa na thamani halisi ya madini hayo.

    Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Adam Ngimba amesema walianza uchimbaji mwaka 2010 na wateja wao wakubwa ni viwanda vinavyotengeneza marumaru na walikubaliana na wateja wao kuchimba na kusafirisha wenyewe kutokana na uchanga wa kampuni yao na kila tani moja hulipwa Sh 3,000.

    Mbali na hayo, pia wananchi walilalamikia sheria ya madini kutofuatwa na kusisitiza kwamba hawajapata faida yoyote wala kusaidiwa mradi wowote licha ya mwekezaji kubeba vifusi vingi.

    Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda aliomba ushirikiano katika idara zote ili kuhakikisha madini yanayochimbwa yanakuwa na faida kwa wawekezaji, serikali na wananchi wake. Hata hivyo, Naibu Waziri alisema wapo watu wanamiliki leseni kiujanja ujanja na kwamba katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, hakuna yeyote atakayedhulumiwa haki yake na kusisitiza kila mtu kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako