• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msingi wa kufanya mazungumzo kati ya China na Marekani ni uaminifu

    (GMT+08:00) 2018-07-26 19:44:30

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo hapa Beijing amesema, tangu Marekani ifanye uchunguzi kwa kutumia kipengele cha 301 dhidi ya China, mara kwa mara China imeeleza kuwa, msingi wa kufanya mazungumzo ni uaminifu, na mpaka sasa, pande hizo mbili bado hazijafanya mawasiliano kuhusu kuanzisha tena mazungumzo.

    Bw. Gao amesema, Marekani kwa kuzingatia ajenda yake ya kisiasa, bila kujali kuharibu mazingira mazuri ya mchakato wa ufufuaji wa uchumi wa dunia na maslahi ya viwanda na watumiaji, imechochea migogoro ya kibiashara, kitendo ambacho ni kinyume na wajibu wake kama nchi kubwa.

    Amesema, kwa mara nyingi China imesisitiza kuwa, haipendi kufanya vita ya biashara, pia haiogopi kufanya vita hiyo, italinda kithabiti maslahi makuu ya nchi na wananchi wake. Vilevile, China itaimarisha ushirikiano wa kibiashara na wenzi wake wa kimataifa, kulinda kwa pamoja kanuni ya biashara huria na mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kuhimiza uchumi wa dunia kuendelea kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako