• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 10 wa kilele wa BRICS wafunguliwa nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-26 20:05:12

    Mkutano wa 10 wa kilele wa nchi zinazoibuka kiuchumi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefunguliwa leo na kutoa wito wa kuboresha uhusiano ili kuinua uwezo wa uzalishaji barani Afrika.

    Afrika Kusini ni nchi mwenyeji wa mkutano huo wenye kaulimbiu "BRICS barani Afrika: Ushirikiano kwa Maendeleo, Ustawi wa Pamoja na Mapinduzi ya 4 ya Viwanda". Viongozi wa nchi wanachama wa BRICS na wajumbe wa biashara wakiwemo wajumbe wa Baraza la Biashara la BRICS, wamehudhuria kikao cha ufunguzi wa mkutano huo, ambao unatarajiwa kujadili juhudi za kina ili kurejesha uhai wa ajenda ya mapinduzi ya viwanda barani Afrika.

    Hii ni mara ya pili kwa Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa BRICS, na inatarajia kutumia nafasi hiyo kuongeza biashara, uwekezaji na uhamishaji wa ujuzi kati ya masoko yanayoibuka na nchi za Afrika ili kunufaika kwa pamoja na ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako