• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa BRICS

    (GMT+08:00) 2018-07-26 21:22:17

    Mkutano wa 10 wa kilele wa nchi zinazoibuka kiuchumi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefunguliwa leo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

    Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutao huo akizihimiza nchi hizo kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Rais Xi amesema, hivi sasa mapinduzi makubwa zaidi ya sayansi na viwanda yanatokea duniani, nchi za BRICS zinapaswa kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati na kuimarisha muundo wa ushirikiano, ili kupata mafanikio ya miaka kumi ya pili. Ametoa mapendekezo manne: kwanza, nchi hizo zinapaswa kuongeza zaidi ushirikiano wa kiuchumi katika sekta za biashara, uwekezaji, mambo ya fedha, mawasiliano ya barabara na nyinginezo. Pili ni kulinda amani na usalama wa dunia kwa msimamo thabiti, kuhimiza migogoro itatuliwe kwa njia ya mazungumzo, na kujenga kwa pamoja uhusiano mpya wa kimataifa wa kuheshimiana na wenye usawa, haki, ushirikiano na mafaniko ya pamoja. Tatu ni kuongeza mawasiliano ya ustaarabu, ili kuongeza maelewano na urafiki wa jadi kati ya wananchi wao, na mwisho, nchi hizo zinapaswa kujenga mtandao wa uhusiano wa wenzi wa karibu, na kuongeza ushirikiano na pande nyingine, ili kutoa mchango zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako