• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waripotiwa kukataa mpango wa Brexit uliotolewa waziri mkuu wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-07-27 08:57:11

    Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza limesema mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit Bw. Michel Barnier, amekataa mpango uliotolewa na waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May na kusema kamwe Umoja wa Ulaya hautakubali mpango huo.

    Bw. Barnier ameweka bayana msimamo wake kwenye mazungumzo ya siku tatu kati yake na waziri mpya wa Brexit wa Uingereza Bw. Dominic Raab. Bw. Barnier pia amesema Uingereza inaweza kujiunga na umoja wa forodha, hatua ambayo inamaanisha kuwa haitakuwa na uhuru wa kufanya makubaliano ya biashara na nchi nyingine duniani baada ya Brexit.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako