• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Houthi wa Yemen watangaza kuushambulia uwanja wa ndege wa Abu Dhabi kwa ndege isiyo na rubani

    (GMT+08:00) 2018-07-27 09:53:58

    Kundi la waasi wa Houthi nchini Yemen limesema ndege yao isiyo na rubani ilishambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi, mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

    Saa moja kabla ya kutolewa kwa tangazo hili la Houthi, mamlaka za uwanja wa Umoja wa Falme za Kiarabu zilikiri kutokea kwa tukio moja, lakini hazikutoa maelezo zaidi.

    Shambulizi hilo kama likithibitishwa litakuwa ni shambulizi la pili la drone kufanywa na kundi la Houthi ndani ya wiki moja.

    Wiki iliyopita waasi wa Houthi walisema ndege yao isiyo na rubani ilikishambulia kituo cha kusafisha mafuta cha kampuni ya Aramco mjini Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako