• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga shutuma za Marekani dhidi ya muundo wa uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:01:10

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Shirika la Biashara Duniani WTO balozi Zhang Xiangchen amesema China inajitahidi kutafuta njia ya uchumi wa soko wa kiujamaa unaoendana na hali yake, na itafuata njia hiyo kithabiti bila kusita wala kujali maoni ya wengine.

    Balozi Zhang amesema hayo katika hotuba aliyoitoa katika mkutano wa tatu wa bodi ya wakurugenzi ya WTO uliofanyika jana mjini Geneva, akipinga waraka wa kushutumu muundo wa uchumi wa China uliosambazwa na Marekani kabla ya mkutano huo.

    Amesema makampuni ya China yanayomilikiwa na serikali yanajiendesha na kuwajibika na faida na hasara zao, uzalishaji kupita kiasi unatokana na kupungua kwa mahitaji kufuatia msukosuko wa kifedha, na China pia haina sheria na kanuni zinazilazimisha uhamishaji wa teknolojia. Pia amesema Marekani imeanzisha vita ya kibiashara na kufanya China ibebe lawama kwa kisingizio cha "muundo wa uchumi wa uharibifu wa China", ili nchi nyingine zinazoogopa kushambuliwa kibiashara na Marekani ziilenge China na kubadilisha ufuatiliaji wa kimataifa, njama hiyo haitafanikiwa.

    Balozi Zhang ameongeza kuwa maendeleo ya China yamenufaisha, na yataendelea kuinufaisha zaidi dunia, na China haijawahi kukanusha kuwepo kwa mapungufu katika mfumo wake wa kiuchumi, na inakaribisha ukosaji na mapendekezo ya kiujenzi, lakini haitapokea shutuma zisizo na msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako