• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachimba madini 650 waokolewa kwenye maafa ya moto chini ya ardhi Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:04:12

    Wachimba madini zaidi ya 600 wameokolewa leo baada ya maafa ya moto kutokea chini ya ardhi katika mgodi wa dhahabu nchini Afrika Kusini. Idara ya madini ya nchi hiyo imesema, ajali hiyo ilianza alhamisi asubuhi kwenye mgodi wa Gold One's Modder Mashariki mwa Springs, katika jimbo la Gauteng.

    Msemaji wa idara hiyo Bw. Nathi Shabangu amesema, wakati wa ajali hiyo, wafanyakazi 644 walikuwa mgodini, na wote wamehamishwa kwenye sehemu ya kukimbilia na kuokolewa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako