• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wapongeza hatua ya mwanzo ya makubaliano ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:08:20

    Msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephan Dujarric amepongeza hatua ya baadhi ya viongozi wa upinzani kuidhinisha makubaliano ya kutatua maswala ya kimsingi yanayohusu kugawana madaraka, kama ni hatua muhimu kwenye mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.

    Hata hivyo Bw. Dujarric amesema hatua ya mwanzo ya kuidhinisha makubaliano hayo, bado kunaacha baadhi ya makundi yakiwa na maswala wanayotilia shaka. Amesema tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini itaendelea kufuatilia mazungumzo yanayoendelea wakati pande zote zinafanya kazi ya kuwa na makubaliano ya amani na shirikishi yaliyo halisi.

    Mgogoro wa Sudan Kusini uliibuka miaka miwili baada ya kupata uhuru kutoka kwa Sudan. Mgogoro huo unaendelea mpaka sasa na umesababisha watu zaidi ya milioni 2.2 kupoteza makazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako