• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Uganda yasema uamuzi wa bunge kuondoa ukomo wa umri wa kugombea urais ni halali

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:08:39

    Mahakama ya katiba ya Uganda imesema uamuzi wa bunge kuondoa ukomo wa umri wa mgombea urais unaendana na katiba. Majaji wanne dhidi ya mmoja, wamesema uamuzi wa bunge kuondoa ukomo wa umri, na kutandika njia kwa rais wa sasa kuwa na uwezekano wa kugombea urais mwaka 2021 kama akitaka, haukinzani na katiba ya nchi.

    Viongozi wa upinzani, na jumuiya za kiraia wamesema hatua ya bunge ilikuwa haramu, kwa kuwa mchakato wa mabadiliko ya katiba kuondoa kipengele hicho, uligubikwa na vurugu na vitisho. Pia wanasema uamuzi huo una lengo la kumwezesha rais wa sasa Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 73, kugombea urais mwaka 2021, atakapokuwa na umri wa miaka 75.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako