• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Marekani ya kusimamisha kwa muda vita vya kibiashara kati yake na Umoja wa Ulaya yalenga kujitafutia faida zaidi

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:23:51

    Rais Donald Trump wa Marekani na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker wameamua kupunguza vikwazo na mikwaruzano ya kibiashara kati yao, na kusimamisha kwa muda kuongezeana ushuru kwa bidhaa za upande mwingine. Kutokana na hali hii, sauti ya kuunga mkono masikilizano kati ya Marekani na Ulaya inaongezeka.

    Lakini kutokana na mabadiliko ya sera yaliyotokea mara kwa mara katika serikali ya Trump, watu wanachukua makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Ulaya kama ni "usimamishaji wa muda wa vita" badala ya "kukomesha vita", na madhumuni yake ni kujitafutia faida zaidi.

    Gazeti ll Washington Post la Marekani limedokeza kuwa, hadi rais Trump alipokutana na Bw. Juncker, baadhi ya washauri waandamizi wa mambo ya uchumi wa serikali ya Trump wanaona rais Trump atatangaza kuongeza ushuru kwa magari yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 yanayoagizwa kutoka nje. Kutokana na hali hiyo inayobadilikabadilika na isiyotabirika, gazeti la the Guardian la Uingereza linamtaja Trump kama mfanyabiashara asiyeaminika. Mwanauchumi wa Marekani pia amesema "labda ujumbe utakaotumwa baada ya dakika 20 kwenye Twitter utageuza hali ya sasa."

    Hivyo njia pekee ya kukabiliana na umwamba wa kibiashara wa Marekani ni ushupavu na upinzani thabiti. Kusalimu amri hakutaweza kuheshimiwa, bali kutahamasisha sera ya Bw. Trump ya "kutoa kipaumbele maslahi ya Marekani", na kuleta hasara kubwa zaidi kwa upande unaojisalimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako