• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jose Mourinho alazimika kukatisha likizo ya beki wake Ashley Young

    (GMT+08:00) 2018-07-27 10:25:23

    Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho, amelazimika kukatisha likizo ya beki wake Ashley Young na kumtaka kurudi kwenda kusaidia safu ya ulinzi ya klabu hiyo kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika mechi za maandalizi. Mourinho amezungumza hayo baada ya mchezo wa International Championship Cup (ICC) wa Manchester United na AC Milan uliopigwa nchini Singapore ambapo katika mchezo huo, United ilishinda kwa penalti 9-8 baada ya kutoka sare ya 1-1. Pia kocha Jose Mourinho amethibitisha kuwa atamruhusu Matteo Darmian kuondoka klabuni hapo watakapopata ofa ambayo wataridhika nayo. Manchester United inakosa huduma ya wachezaji wake muhimu katika safari yake ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, wachezaji ambao bado wako likizo ni Ashley Young, David de Gea na Romelo Lukaku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako