• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za BRICS zahimiza kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-07-27 15:07:00

    Mkutano wa kumi wa viongozi wa nchi za BRICS umefanyika huko Johannesburg. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mkutano wa baraza la viwanda na biashara la nchi za BRICS huku akisisitiza kuwa, wakati uchumi wa dunia unakabiliwa na mabadiliko makubwa, ufunguaji mlango ni njia pekee inayonufaisha nchi tofauti, kuleta ustawi wa pamoja na maendeleo ya kudumu, na ni chaguo la busara nchi mbalimbali lenye busara.

    Viongozi wengine pia wameonesha nia ya kushikilia ushirikiano wa ufunguaji mlango wazi na kutafuta maendeleo ya pamoja. Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema hatua ya upande mmoja na ulinzi wa biashara zitaleta athari mbaya kwa maendeleo ya dunia nzima, huku akisisitiza kuwa nchi za BRICS ni mhimizaji na mlinzi wa mfumo wa biashara.

    Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara ya nchi za BRICS Bw. Iqbal Surve, amesema biashara huria ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya nchi za BRICS na dunia nzima, na nchi za BRICS zitashirikiana kukabiliana na kujilinda kibishara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako