• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na Afrika yaongezeka

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:53:13

    Biashara kati ya China na Afrika imefikia dola za kimarekani bilioni 99.84 ndani ya kipindi cha miezi sita mwaka huu ikiwa ni juu kwa asilimia 17 ikilinganishwa na mwaka uliopita.Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, bidhaa za China zilizoingia Afrika ziliongezeka na kufikia asilimia 8.1 ikiwa ni sawa na dola bilioni 50.37 huku bidhaa za Afrika zilizosafirishwa China zikiongezeka na kufikia asilimia 28.6 ikiwa ni sawa na dola bilioni 48.47. Mwezi Juni pekee, biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 16.82 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Hata hivyo katika kipindi cha miezi sita mwaka huu ukuaji wa biashara kati ya China na Afrika ulikuwa chini ikilinganishwa na nchi za Marekani Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako