• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kujenga soko kubwa katika Chaka kaunti ya Nyeri

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:53:47

    Serikali ya Kenya imetoa hakikisho kwa wenyeji wa Kaunti ya Nyeri kuwa soko la Chaka ambalo limetengewa Sh135 milioni litajengwa katika kipindi hiki cha matumizi ya fedha za serikali cha 2018/19. Akitoa hakikisho hilo, katibu maalumu katika Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi, Bw Hinga Mwaura, amesema kuwa soko hilo haliko katika orodha ya miradi ambayo rais Uhuru Kenyatta alipiga marufuku ya utekelezaji.

    Katika marufuku hiyo, rais alitangaza kuwa hakuna miradi mingine mipya itafadhiliwa kabla ya ile ambayo imebakia imekwama imalizike kwanza.

    Bw Mwaura ameongeza kuwa soko hilo liliwekwa katika mtandao wa ufadhili mwaka wa 2007 lakini ukosefu wa fedha ukalifanya likose ufadhili. Mwaura amesema kuwa soko hilo liko na umuhimu sana kwa uchumi wa kitaifa na ule wa Kaunti ya Nyeri kwa kuwa linahudumia wachuuzi zaidi ya 1,000.Alisema kuwa ni soko ambalo limesaidia sana uthabiti wa pato la Mji wa Chaka na lina manufaa sana kwa wateja ambao hutegemea bidhaa za kilimo ambazo huuzwa kwa bei nafuu katika soko hilo lililo katika barabara kuu ya kutoka Marwa kwenda Nanyuki ukipitia Naromoru.

    Bw Kega alisema kuwa kukwama kwa soko hilo kumekuwa kukizua changamoto tele kwa wateja, wachuuzi na hata pia kwa wanasiasa wa eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako