• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yamtaka mkandarasi kufuata mkataba kikamilifu

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:54:03

    Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wa Tanzania Selemani Jafo amemtaka mkandarasi anayejenga stendi na soko la kisasa la kimataifa jijini Dodoma, kutekeleza miradi hiyo vizuri kwa kufuata mkataba na kuwa hakutakuwa na muda wa kuongezwa kukamilisha kazi hiyo.

    Amesema hayo alipotembelea eneo inakojengwa stendi hiyo Nzuguni, ambalo sasa mkandarasi yuko katika maandalizi ya awali ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo, ambayo itachukua miezi 15 ili kukamilisha.

    Hadi hapa amesema ameridhishwa na maandalizi ya awali, ikiwa ni muda mfupi tangu watie saini makubaliano. Kwa upande wake, mhandisi wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Manyanga amesema eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga soko hilo lenye ghorofa moja ni ekari 30 wakati stendi ya kisasa imetengewa eneo la ekari 87. Shilingi bilioni 77.8 zimetengwa kwa ujenzi wa stendi ya kisasa, soko na uboreshaji wa miundombinu ya barabara hizo.

    Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema jiji limezungumza na kampuni ya Kikorea kuweka taa na kamera za usalama katika barabara kuu za Iringa, Singida, Arusha na Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako