• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano usio rasmi wa kuadhimisha miaka 10 tangu kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa viongozi wa BRICS wafanyika

    (GMT+08:00) 2018-07-27 19:41:13

    Mkutano usio rasmi wa kuadhimisha miaka 10 tangu kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefanyika leo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

    Mkutano huo umehudhuriwa na rais Xi Jinping wa China, rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, rais Michel Temer wa Brazil, rais Vladmir Putin wa Russia na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi.

    Akihutubia mkutano huo, rais Xi amesema katika miaka 10 iliyopita, BRICS imekuwa mfumo wenye ushawishi mkubwa wa ushirikiano wa kimataifa, na katika miaka 10 ijayo, nchi za BRICS zinapaswa kufuata kanuni ya amani na maendeleo, na kutumia fursa ya mapinduzi mapya ya tekenolojia na viwanda, ili kuanzisha miaka 10 ya pili yenye mafanikio makubwa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa kifunguo cha maendeleo ya ushirikiano wa BRICS ni kujiendeleza zaidi, kuboresha maisha ya wananchi, na kujitahidi kupata amani ya kudumu, usalama, ustawi wa pamoja, ufunguaji mlango na dunia yenye mazingira mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako