• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema uchumi wa China utaongezeka kwa asilimia 6.6 kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-27 19:50:29

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limekadiria kuwa uchumi wa China utaongezeka kwa asilimia 6.6 kwa mwaka huu, na kwamba China imepata maendeleo makubwa katika sekta muhimu za kuimarisha usimamizi wa fedha na kuhimiza ufunguaji mlango wa kiuchumi.

    Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na IMF jana baada ya kufanya majadiliano na China kuhusu "kipegele cha nne", na kupongeza mkakati wa China unaotilia maanani zaidi ongezeko la ubora kutoka ongezeko la kasi. Pia Shirika hilo limesifu maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya mageuzi, hasa kuchukua hatua ya kupunguza hatari za mambo ya fedha na kuendelea kuhimia ufunguaji mlango wa kiuchumi.

    IMF imesema inapaswa kujenga mfumo wa jumla kuhusu pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, kuboresha uratibu na usimamizi, kuchukua njia wazi ya ununuzi, na kufuatilia uwezo wa kulipa madeni wa nchi za kirafiki, hatua ambazo zitasaidia kufanikiwa kutekeleza pendekezo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako