• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa ushirikiano wa Asia ya Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-07-27 19:52:59

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang Leo amesema, kuanzia tarehe 31 Julai hadi tarehe 5 Agosti, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara nchini Malaysia na Singapore, na kuhudhuria mikutano ya mawaziri wa mambo ya nje ya ushirikiano wa Asia ya Mashariki.

    Bw. Geng Shuang amesema, Bw. Wang Yi atabadilishana maoni na wenzake wa Asia ya Mashariki kuhusu uhusiano kati ya China na Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini na Mashariki, ushirikiano wa Asia ya Mashariki na masuala yanayofuatiliwa na pande mbalimbali.

    Amesema, ushirikiano wa kanda ya Asia ya Mashariki ni jukwaa muhimu la kufanya mazungumzo, kuimarisha ushirikiano na kuhimiza maendeleo kwa nchi za kanda hiyo. China inatumai mikutano hiyo itafuatilia ushirikiano, kupanua maoni ya pamoja, na kusukuma mbele maendeleo na ushirikiano wa kanda hiyo, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako