• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria lakaribia eneo linalodhibitiwa na kundi la IS kusini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2018-07-27 19:55:27

    Jeshi la Syria limepata maendeleo makubwa katika mapigano dhidi ya kundi la IS katika eneo la bonde la Yarmouk, mkoa wa Daraa ulioko kusini mwa Syria.

    Jeshi hilo limedhibiti mabwawa ya Wadi Saisun na Sahem al-Golan baada ya mapambano na wapiganaji wa kundi la IS kwenye bonde la Yarmouk mapema leo. Mafanikio hayo yamepatikana baada ya jeshi hilo kudhibiti mlima muhimu wa Tal al-Gumou na miji ya Jalin, Hait, Tsil na mji wa Edwan katika eneo la bonde hilo.

    Shirika la Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake makuu Uingereza limesema hivi karibuni kuwa, asilimia 90 ya mkoa wa Daraa inadhibitiwa tena na jeshi la serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako