• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • COMESA yapeleka waangalizi katika uchaguzi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-07-27 20:21:45

    Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) imepeleka waangalizi wa muda mfupi katika uchaguzi utakaofanyika jumatatu wiki ijayo nchini Zimbabwe.

    Kabla ya kupelekwa waangalizi hao 19 walipewa mafunzo ya kina ili kuwapatia uelewa wa mfumo wa kisheria wa Zimbabwe na pia ujuzi na uwezo wa kufuatilia uchaguzi.

    Wakati huohuo, Ujumbe wa Kufuatilia uchaguzi wa Umoja wa Ulaya umepeleka waangalizi 44 katika maeneo yote nchini Zimbabwe kufuatilia uchaguzi huo. Kabla ya kupelekwa nchini Zimbabwe, waangalizi hao walipewa mafunzo ya kina ya siku mbili kuhusu historia ya uchaguzi, mchakato wa kupiga kura, mazingira ya kisiasa na mambo mengine muhimu yanayoendana na majukumu yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako