• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahudhuria mazungumzo ya viongozi wa BRICS+

    (GMT+08:00) 2018-07-27 21:45:20

    Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mazungumzo ya viongozi wa BRICS+ yaliyofanyika leo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

    Katika hotuba yake, Rais Xi amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mapinduzi, maendeleo na marekebisho makubwa, nchi zinazoibuka kiuchumi na nchi zinazoendelea zina fursa ya pamoja, huku zikikabiliwa na changamoto ya pamoja, hivyo ni muhimu kwa nchi hizo kuongeza mshikamano na ushirikiano. Amependekeza pande hizo mbili kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kunufaishana, kutafuta injini mpya ya maendeleo, kuanzisha mazingira mazuri ya nje na kujenga uhusiano mpya wa kimataifa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, bila kujali maendeleo makubwa kiasi gani yamepatikana, China itakuwa pamoja na nchi zinazoendelea daima, na kuunga mkono nchi hizo kupata maendeleo, na kudumisha uhusiano wa wenzi wa karibu nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako