• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo kutokana na tetemeko la ardhi nchini Indonesia vyafikia 10, na 40 wakijeruhiwa

    (GMT+08:00) 2018-07-29 16:40:25

    Shirika la kukabiliana na majanga la Indonesia Widyamotko limetoa taarifa kuwa watu 10 wamefariki na wengine 40 wakijeruhiwa jumapili hii katika jimbo la Magharibi la Nusa Tenggara kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 katika kipimo cha Richta.

    Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa, 9 kati ya 10 waliofariki ni raia wa Indonesia na mmoja kutoka Malaysia, na kwamba vifo hivyo vimesababishwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na tetemeko hilo, na kuna hofu kuwa huenda idadi ya waathirika ikaongoezeka kwa kuwa mpaka sasa vikosi vya uokozi vinaendelea na kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako