• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano kati ya Marekani na Ulaya yatajwa kutohusiana na biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-07-30 08:48:26

    Mbunge mmoja wa Ujerumani amesema makubaliano yaliyosainiwa kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya yanalenga kuiridhisha Marekani, na hayahusiani hata kidogo na biashara huria.

    Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kigeni ya Bunge la Ujerumani kwa chama cha upinzani cha AfD Bw. Petr Bystron, amesema kwenye makubaliano hayo rais Donald Trump amepata yote anayotaka, na kwamba bila kujali makubaliano yana manufaa gani kwa Umoja wa Ulaya, uamuzi wa kununua gesi na maharage ya soya kutoka kwa Marekani unatia shaka.

    Jumatano iliyopita rais Trump na mwenyekiti wa kamisheni ya Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker walifikia makubaliano ya kuepuka vita kamili ya kibiashara, na Ulaya itanunua gesi na maharage ya soya kutoka Marekani, ili Marekani ifute mpango wa kutoza ushuru dhidi ya magari ya Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako