• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la ngoma za jadi la Afrika lafunguliwa nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-07-30 09:16:06

    Tamasha la kumi la ngoma za kienyeji za Afrika limefunguliwa katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku tano hadi Agosti 3 na kuvutia washiriki kutoka nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Afrika.

    Wasanii kutoka Rwanda, Burkina Faso, DRC na Senegal watafanya maonyesho katika miji mbalimbali ya Rwanda, kabla ya sherehe za kufungwa kwa maonyesho hayo kusini mwa Rwanda.

    Maonyesho ya ngoma za kienyeji ya Afrika yalizinduliwa na Umoja wa Afrika mwaka 1998, kwa lengo la kuwaleta pamoja waafrika na kuhimiza utamaduni wa amani kupitia ngoma za jadi za Afrika. Mwaka huu tamasha hili linafanyika pamoja na siku ya kutoa shukrani ya Rwanda, Umuganura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako