• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema inaweza kukabiliana na vikwazo vya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-30 09:48:03

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amesema watu wa Iran iwanaweza kupita kipindi "kigumu" cha sasa katika kukabiliana na tishio la vikwazo vyaitakavyotolewa na Marekani.

    Akinukuliwa na televisheni ya Press TV ya Iran, Bw. Zarif amesema Marekani ina uraibu wa kutoa vikwazo , na historia ya uhusiano wa Marekani na nchi za nje imeonyesha kuwa nchi hiyo imewekatoa vikwazo dhidi ya nchi nyingi duniani.

    Ameongeza kuwa Iran inaweza kugeuza mashinikizo kuwa motisha ya kuongeza uzalishaji wa kitaifa na uuzaji bidhaa zisizo mafuta nje ya nchi, na kuiambia Marekani kuwa inapaswa kuacha kutumia mbinu yake ya kutumia vikwazo.

    Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vitaanza kutekelezwa mwezi Agosti na Novemba, hatua iliyotangazwa baada ya Marekani kujitoa kwenye Makubaliano ya Nyuklia ya Iran Mei, 8.

    Habari nyingine zinasema bei yza mafuta zimelipanda juu kidogo katika wiki iliyopita, kutokana na tishio la rais Donald Trump wa Marekani la kuiwekea vikwazo Iran na nchi nyingine zenye uhusiano wa kibiashara na Iranyo, utoaji mpya wa mafuta kutoka Shirika la Nchi Zinazosafirisha Mafuta kwa Wingi Duniani OPEC, na kupungua kwa mahitaji ya nishati kufuatia mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China na nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako