• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wananchi wa Mali wapiga kura kumchagua Rais

    (GMT+08:00) 2018-07-30 09:54:28

    Watu zaidi ya milioni 8.4 wa Mali wamejitokeza kupiga kura kumchagua rais wao mpya.

    Upigaji kura ulianza jana saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa saa za huko, na kufanyika katika hali ya utulivu, isipokuwa vituo vya kupigia kura katika sehemu za kaskazini na katikati mwa Mali vimeshambuliwa na wapiganaji wasiojulikana.

    Waangalizi zaidi ya elfu sita kutoka ndani na nje wamesimamia mchakato mzima wa upigaji kura.

    Wagombea urais 24 wanashiriki kwenye uchaguzi huo, vyombo vya habari vya Mali vinaona ushindani mkali utakuwa ni kati ya rais wa sasa Bw. Ibrahim Keita na mgombea wa chama cha upinzani Bw. Soumaila Cisse. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako