• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kombe la CAF: Gor Mahia yaishinda Yanga, sasa yaongoza kundi D

  (GMT+08:00) 2018-07-30 11:08:13

  Gor Mahia ya Kenya jana imefanikiwa kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwa kuifunga 3-2 Yanga ya Tanzania iliyokuwa nyumbani mjini Dar es Salaam.

  Magoli ya Gor Mahia kwenye mechi hiyo yalipatikana kupitia George Odhiambo, Jacques Tuyisenge na Haruna Shakava, huku magoli mawili ya kufutia machozi ya Yanga ambao sasa hii ni mechi ya tatu wanafungwa katika mechi nne walizocheza yalifungwa na Deus Kaseke pamoja na Rafael Daudi.

  Kwa ushindi huo, Gor sasa wanafikisha pointi 8 na kuongoza kwenye msimamo wa kundi D licha ya kuwa wanalingana alama hizo na USM Algiers ya Algeria.

  Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa jana mjini Blida nchini Algeria, Rayon Sport kutoka Rwanda waliwalazimisha sare ya magoli 1-1 wenyeji USM Algiers.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako