• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio Mchanganyiko, Rwanda kuandaa mashindano ya kimataifa ya Afrika wiki ijayo

    (GMT+08:00) 2018-07-30 11:08:37

    Rwanda inatarajia kuandaa mashindano ya siku moja ya Kombe la Ubingwa wa Afrika la mbio mchanganyiko (African Triathlon Cup), zitakazofanyika mjini Rubavu Agosti 4 mwaka huu.

    Akitibitisha hilo, Rais wa shirikisho la Triathlon la Rwanda Alexis Mbaraga amesema jumla ya wanamichezo 32 wamejisajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zitakazojumuisha hatua tatu, kuogelea umbali wa mita 750, mbio za baiskeli umbali wa kilomita 20, na riadha umbali wa kilomita 5, vyote kwa pamoja na kwa wakati mmoja.

    Mbali na Rwanda, nchi nyingine zilizotoa washindani ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Kenya, Namibia, Niger, Jordan, Marekani, Mauritius, na Australia.

    Michuano hiyo pia itatumika kukusanya alama zitakazowasaidia washiriki hao kufuzu mashindano ya olimpiki ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako