• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Usajili wachezaji: AS Kigali yathibitisha kumsajili Elias Maguri wa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-07-30 11:08:59

    Kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kujiimarishwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini Rwanda, timu ya AS Kigali imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Elias Maguri aliyekuwa anacheza klabu ya Dhofar SC ya Oman.

    Maendeleo ya Usajili huo, yalithibitishwa na meneja wa AS Kigali Joseph Nshimiye aliyesema mchezaji huyo sasa anaingia mkataba wa miaka miwili na timu hiyo.

    Katika msimu uliopita wa ligi, AS Kigali ilijikusanyia alama 61, na ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya mabingwa APR.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako