• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Magari ya Mwendokasi: Hamilton ashinda mbio za Hungary

    (GMT+08:00) 2018-07-30 11:09:18

    Dereva wa magari ya mashindano ya mwendokasi Lewis Hamilton wa Uingereza jana ameshinda mbio za Hungary na kumfanya ajiongezee nafasi kwenye kinyang'anyiro cha kutwaa ubingwa wa jumla msimu huu, kwa kuwa sasa amefikisha alama 213 ambazo ni 24 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sebastian Vettel wa Ujerumani.

    Katika mbio hizo za jana, Vettel ambaye ni kutoka timu ya Ferari alikamata nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilikamatwa na dereva mwingine wa timu ya Ferari Kimi Raikonnen wa Finland.

    Kati ya mbio 12 zilizokwishafanyika, Hamilton ameshinda 5 na madereva hao kwa sasa watapumzika, kabla ya kuendelea na mbio 9 zilizosalia msimu huu, wakitarajia kukutana Agosti 24 kwenye mbio za Ubeligiji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako